28 Aprili 2025 - 22:51
Source: Parstoday
Mwislamu auawa Ufaransa, muuaji alirekodi uhalifu huo na kumtukana Mungu

Muislamu mmoja ameuawa nchini Ufaransa baada ya kudungwa kisu takriban mara 50 na mwanamume Mfaransa mwenye chuki dhidi ya Uislamu ndani ya msikiti katika manispaa ya La Grand-Combe katika eneo la Le Gard kusini mashariki mwa Ufaransa. Polisi wamemtambua mtu huyo.

Gazeti la Ufaransa la Le Figaro limeripoti kwamba wachunguzi waligundua video ambayo mhalifu huyo alijirekodi wakati akitenda uhalifu huo, ambapo anamtukana raia huyo Muislamu na kumtusi Mwenyezi Mungu kwa lugha chafu.

Gazeti hilo limemnukuu Mwendesha Mashtaka wa Umma wa Jamhuri katika eneo la Alice, Abdelkarim Grini, akisema kwamba alikuwa akichunguza "dhana zote, ikiwa ni pamoja na dhana ya hujuma dhidi ya Uislamu."

Muuaji hakujua kuwa kamera za ulinzi za msikiti huo zilikuwa zikimrekodi hadi alipokamilisha uhalifu huo na ndipo alipofoka: "Nitakamatwa, ni hakika!" na kisha akakimbia. Mhalifu huyo alikamatwa muda mfupi baadaye.

Baada ya kuchunguza utambulisho wake, polisi ya Ufaransa imebaini kuwa raia huyo si Muislamu.

Uhalifu huo ulifanyika Ijumaa asubuhi ndani ya msikiti huo. Mwathiriwa, mwenye umri wa kati ya miaka 23 na 24, hakupatikana hadi waumini walipoanza kuwasili msikitini hapo kwa ajili ya Swala ya Ijumaa. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha